Wednesday, April 25, 2012

Prezzo PK atlast



Peter Kenneth ambaye ni mbunge wa Gatanga amejitokeza kama mgombezi wa kiti cha urais nchini Kenya na Chama chake cha KNC . Peter Kenneth amezidua campeini yake leo tarehe 4/11/2012 na natarajia kuwa Wakenya watamuunga mkono.

 Kwa maoni yangu, PK anafaa kuchaguliwa kama Rais wa Kenya kwa Hali na Mali.
Katika ulingo wa kisiasa kuna mengi ambayo yanaendelea huku vita vya maneno kati ya Waziri mkuu Raila Odinga na Kinara wake Uhuru Muigai. Siasa za Nchi zilipiga mwelekeo mpya wakati Mahakama ya Haugue ilipowataja Bwana Uhuru Muigai na William Ruto katika mashtaka ya PEV 2007. Siasa za Kenya zinaelekea kuwa za kikabila huku wananchi wengi wa kutoka kwenye jamii ya Agikuyu wakiunga Uhuru Muigai, Jamii ya Waluo wakiunga Raila Odinga nao Wakalejin wakiunga William Ruto. Swali kubwa ni, Mbona kila kabila linaunga mmoja wao ilihari hawa viongozi ndio kiini cha shinda zilizoko Kenya?
Ni wakati wa Wakenya kuungana mikono maana shinda zilizoko Kenya hazijui Kabila. Kuna kabila mbili tuu nchini Kenya. Kambila la kwanza ni la Matajiri nalo kabila la pili ni La Masikini. Tukiangalia Kwenye mseto wa Hospitali, Shule na Makao utaona ya kwamba hamna hospitali za kabila fulani ila hospitali za matajiri. Mashule vile vile yanasajili kila mwanafunzi lakini kuna mashule ambayo yanasajili wanafunzi waliotoka kwenye familia zenya mali. Wakenya wote wanaishi kila mahali kwa Amani bila ukabila lakini kuna Maeneo ambayo sio ya wakenya wowote ila walio na mali.

 Sote kama wakenya Tunahitaji Maendeleo. Tunahitaji kiongozi ambaye ataleta mwelekeo mpya nchimi mwetu. Kiongozi ambaye sera zake zitawafanya waliomasikini kupata angalao nafasi ya kusahau umasikini. Kiongozi ambaye ataendeleza nchi ili wazazi wapate nafasi ya kupata mali na kuwapeleka watoto wao katika shule ambazo wangetaka. Kiongozi ambaye ndoto yake ni Kenya na sio Kabila. Haya yote yanaweza fikiwa watu wote wakiungana na kupiga Ukabila marufuku. Shinda zinazowakumba wakenya ni sawa kila mahali, ni muhimu basi kuchaguwa kiongozi mzuri.

Kwangu naona Pk ni kiongozi shupavu, tukiangalia wagombezi Urais wote utaona ni Pk tu ambaye ameendeleza eneo lake la Mbunge kupitia CDF kwa jia mzuri. Wengi wanaogommbea Urais wamehusishwa na kashfa mingi ambazo zinahusu utumiaji mamlaka vimbaya, hongo na pia siasa mbovu.

Wakenya tugutuke na Pk. Mungu abariki Kenya. Kenya Moja milele. Tazama Video ya Gatanga cdf hapa.